Muhtasari Halisi wa Betway Nchini Kenya

Karibu Bonasi
Sasisho la mwisho kutoka kwa Efirbet :

Kuhusu Betway

Kampuni ya kamari ya Betway ni mojawapo ya kampuni ambazo zimenawiri katika mchezo wa Kamari mtandaoni. Kampuni hii ilianzishwa nchini Malta mwaka 2006 na inaendeleza kamari kwa Michezo ya Mpira, Bingo, Vegas na Poker miongoni mwa michezo ingine.

Kampuni ya Betway inafanya kazi katika soko zilizodhibitiwa na zilizo na leseni katika mataifa tofauti tofauti. Baadhi ya mataifa haya ni Uhispania, Italia, Uingereza, Malta, Ireland, Sweden, Ujerumani, Denmark na Ubelgiji. Hata hivyo, kampuni hii imejikwachulia umaarufu miongoni mwa nchi za Kiafrika kama vile Afrika Kusini na Nigeria.

Nchi ya Kenya haijaachwa nyuma katika maaliko ya Kampuni ya Betway katika ulingo wake wa kamari. Humu nchini, Betway ilisajilishwa na Kamati ya Kusajili na Kudhibiti Kamari (BCLB) mwaka wa 2015. Lengo kuu la kuisajili lilikuwa ni kuwapa wakenya nafasi mpya ya kuwekeza dau katika Kamari.

Hili linamaanisha ya kwamba wakenya wangepata nafasi ya kuwekeza kwa odi nzuri na soko murwa za kuwekeza dau zao.


Jinsi ya Kujisajilisha katika Betway

Njia ya usajili wa Betway

Ili uweze kushiriki Kamari katika tovuti ya kampuni yoyote ile, unahitaji kufungua akaunti na kampuni hiyo. Akaunti hiyo ndiyo itakayokuwezesha kushiriki katika mchezo, kutazama mapato yako kutokana na kamari uliyoshiriki na vile vile kuchagua kiwango cha kuwekeza. Katika Betway vile vile, unahitaji kutengeneza akaunti ili uweze kucheza kamari.

Unahitajika kujaza baadhi ya maelezo yako ya kibinafsi ili kutengeneza akaunti yako katika tovuti ya Betway. Ni vyema utoe maelezo ya kweli pasi kundanganya kwa lolote usije ukawa na ugumu utakapokuwa unabihi mapato yako.

Hakikisha umefuata hatua zifuatazo katika usajili wako kwa Kampuni ya Betway nchini Kenya;

 1. Fungua Betway
 2. Bonyeza sehemu iliyo na chaguo la ‘jisajili’ katika tovuti ya Betway
 3. Jaza nambari yako ya rununu
 4. Buni nywila yako
 5. Jaza baruapepe yako na majina kama yanavyofaa kufuatana
 6. Jaza kodi ya kujisajili kama unayo
 7. Weka alama katika sehemu ya hakikisho ili kudhibitisha wewe ni wa umri ufaao na kwamba umekubaliana na sheria na masharti ya Betway
 8. Bonyeza sehemu inayofuata ili kuchagua aina ya kitambulisho na kisha ujaze nambari yake, tarehe ya kuzaliwa, na uraia
 9. Bonyeza sehemu ya kujisajili ili kutengeneza akaunti yako

Baada ya kujisajili, ni lazima utembelee tovuti ya Betway Kenya kila wakati unapotaka kuingia kwenye akaunti yako.

Sajili huko Betway


Muundo wa Tovuti – Rasimu na Uabiri

Ukurasa wa nyumbani

Kampuni ya Betway nchini Kenya inakupa tovuti unayoweza kuitumia kwa urahisi mkubwa kila wakati. Rasimu ya tovuti yenyewe ina kiolesura cha kupendeza kiasi kwamba yeyote anaweza kuitumia bila ugumu.

Kampuni ya Betway ina uabiri wa kimuundo unaoukupa fursa ya kuziabiri kurasa za kimtandao kwa utaratibu kulingana na mpangilio wake. Hili ni jambo la manufaa kwa mcheza kamari kwani ukurasa mmoja unakuelekeza kwa mwingine ambao una maelezo na uhondo zaidi.

Hatimaye, unagundua umeziabiri kurasa zote za tovuti zilizo na taarifa ulizokuwa ukitafuta. Kumbuka kuwa kabla uufungue ukurasa unaofuata, utakuwa umesoma kurasa nyingine kadhaa na hivyo utakuwa na ujumbe unaokutosha kuwekeza dau katika mchezo.

Tovuti ya Betway inasisimua na vile vile ina mvuto fulani kwa anayeitumia.


Kamari ya Michezo ya Mpira

Kitabu cha michezo cha Betway

Kampuni ya Betway ina baadhi ya sehemu za kuwekeza dau. Unafaa kuchagua mchezo ambao ungependa kuuwekezea dau na mojawappo ya sehemu hizi ni dau zinazohusu michezo ya mpira.

Sehemu hii ina michezo kadhaa ambayo unaweza kuiwekezea dau. Baadhi ya michezo hii katika kitengo hiki ni kama kriketi, mchezo wa magongo kwenye barafu, mpira wa vikapu, mpira wa kadanda na tenisi.

Soko za Kuwekeza Dau

Soko za kuwekeza dau katika michezo tofauti tofauti zina baadhi ya chaguo ambazo unaweza kuziwekezea dau. Una nafasi ya kuchagua kama wataka michezo itakayochezwa baadaye au inayofanyika kwa sasa. Katika kila mchezo, kuna soko zifuatazo za kuwekeza;

 • Magoli sahihi. Huu ni utabiri wa matokeo ya mechi yote
 • Timu itakayofunga goli kwanza. Utabiri wa timu itakayotangulia kufunga goli kwa muda wa dakika 90
 • Matokeo ya kipindi cha kwanza/kipindi cha pili. Utabiri wa matokeo ya kila kipindi kwa usahihi
 • Matokeo ya mwisho wa mechi
 • Kutabiri kuhusu magoli hasi
 • Sare ya magoli
 • Ukosefu wa sare katika mechi
 • Uwezekano wa timu moja kushinda mechi au kutoka sare
 • Kutabiri mchezaji atakayekuwa wa kwanza kufunga goli na idadi ya magoli katika mechi

Hatimaye, kuna zawadi kuu ya jackpoti ambayo hutuzwa mshindi kila wiki . Hii ndiyo zawadi kubwa zaidi ambapo mshindi anafaa kutabiri mechi 13 kwa usahihi. Jakpoti hii ni ya Shilingi 10, 000, 000. Vile vile, kuna jakpoti aina nyingine ambapo kuna mechi sita pekee.

Odi

Ikilinganishwa na kampuni nyingine za michezo ya kamari zilizopewa kibali na BCLB, Betway ni mojawapo ya kampuni ambazo huwapa wachezaji wake odi za juu. Hata hivyo, Unafaa kuwa makinifu mno unapozichagua timu za kuwekea dau kwa maana uwezo na ustadi wa timu uwanjani huathiri odi.

Betway huwapa wateja wake odi za aina tatu. Odi hizi ni zile za Nukta, Akisami na za Kimarekani.


Zawadi ya Betway ya Kuwakaribisha Wateja wa Kenya-50% hadi Shilingi 5, 000

Betway inakaribisha ziada kwa wachezaji wa Kenya

Kufikia sasa, tayari tumejua utaratibu wa kujisajili na Betway nchini Kenya. Taarifa ya kuvutia wateja ni kwamba, ukifaulu kujisajili na kampuni hii na uweke amana yako ya kwanza kwenye akaunti yako, unapata bakshishi ya asilimia 50 kwenye akaunti yako. Bakshishi hii inatolewa hadi shilingi 15, 000, hivyo ni kama utawekeza dau bure bilashi. Naam, unacheza kamari ya pesa za bure!

Bakshishi hii inahitaji uitumie katika kuwekeza dau kwa mara tatu na timu zako ziwe na odi zaidi ya tatu. Hata hivyo, ukiwekeza dau katika michezo ya casino au michezo isiyo halisi (virtual games), hazitachangia kufuzu kwako kupewa bakshishi hii.

Pata Bonasi yako


Uwekezaji Dau wa Moja kwa Moja

Betway kuishi bets

Kwa wale wenye ari kubwa ya kufuata timu za mpira wa kandanda na ligi, Betway inakutolea fursa ya kufuata mchuano huo kupitia sehemu hii. Unapohitaji kuwekeza dau, unahitaji kuitembelea tovuti ya Betway nchini Kenya na ufungue sehemu ya michuano ya moja kwa moja. Kisha, chagua mechi moja inayokupendeza na baadaye unaweza kuwekeza dau bila wasi wasi.

Baadaye, fanya uamuzi wa kiwango cha fedha ambacho ungetaka kuwekeza na kisha ufanye hivyo.

Wakati mwingine kujitazamia jinsi timu yako inavyocheza uwanjani kunakupa msisimko mkubwa. Hata hivyo, kutazama huku kunaweza kupa dhiki au hata faraja kwani unajitazamia jinsi mchuano ulivyo. Tayari, unaweza kuyafanya makadirio yako ili kujua kama utashinda au utashindwa kwenye kamari hiyo.

Katika hii sehemu ya michuano ya moja kwa moja, una nafasi nzuri ya kujionea matokeo ya michuano inayoendelea uwanjani pamoja na wakati wake. Hivyo, unaweza ukafanya uamuzi wa kuwekeza dau mpira unapoendelea.


Utoaji wa Fedha Kabla ya Mechi Kukamilika

Wakati mwingine unapowekeza dau, unahitaji kubihi pesa zako hata kabla ya mchezo kuisha. Kampuni ya Betway inakupa nafasi hii. Hili linakupa nafasi ya kubihi pesa ulizowekeza kabla ya kipindi cha dakika 90 kukamilika.

Kulingana na jinsi mchezo ulivyo wakati wa kutoa fedha ulizowekeza kabla ya mchezo kuisha, unaweza kupata faida au hata hasara vile vile. Baada ya kubihi fedha zako, zitaingia kwenye akaunti yako ya Betway Kenya. Kwa ujumla, kiwango cha pesa zitokanazo na ushindi wako kinategemea odi zilizo sokoni kufuatia mchezo uliokuwa umeuwekezea dau. Ni vigumu sana kupata fedha nyingi zaidi katika mechi zaidi ya zile ambazo ungezipata kufuatia odi zilizotolewa mwanzoni wa mchezo ule.

Chaguo hili la kutoa fedha ulizoziwekeza kabla ya mchuano kukamilika linakupa fursa kuahirisha uwekezaji wa dau baada ya kubadili wazo lako. Vile vile, linakusaidia unapoamua kupunguza hasara ambayo ungeipata kutokana na mchuano fulani.


Utazamaji wa Michuano ya Moja kwa Moja

Kampuni ya Betway inakupa fursa ya kujitazamia na kufuatilia matukio uliyoyachagua. Chaguo la michezo endelevu kwa sasa linautia uwekezaji dau msisismko. Hata hivyo, chaguo hili la kutazama michuano ya moja kwa moja halipatikani katika Betway kwa wachezaji wa Kenya ila tu lipo kwa michezo michache iliyochaguliwa.

Michezo iliyopewa kipaumbele kuonyesha matukio halisi na kwa wakati yanapotendeka ni kama rugby, kandanda, mchezo wa makapu, mpira wa magongo na tenisi vile vile. Katika hii michezo, angalau unaweza kupata nafasi ya kufanya uchambuzi mzuri kabla ya kuwekeza dau lako. Licha ya kuwa kuwekeza dau kwa matukio yanayoendelea sio kwa michezo yote, angalau una kiini kizuri cha kujipatia matukio yote kuhusiana na mchezo unaoendelea kwa muda huo. Matukio haya ni kama idadi ya magoli yaliyofungwa, idadi ya shoti elekevu, na vile vile asilimia za umiliki wa mpira kwa kila timu uwanjani.

Kuna nafasi ya kutazama michuano inayofanyika moja kwa moja katika Betway. Hapa nchini, una nafasi ya kutazama tu matukio maarufu kwa njia ya moja kwa moja humu nchini. Tutazidi kukupasha kuhusu mabadiliko yoyote ambayo yanaweza kujitokeza pindi tu yanapotukia.


Sehemu ya Casino ya Betway

Kasino ya Betway

Kampuni ya Betway nchini Kenya ina sehemu ya casino inayokupa nafasi ya kujivinjari kwa kushiriki katika michezo anuwai tovutini. Baadhi ya michezo ambayo unaweza kuchagua katika sehemu hii ni video poker, table games, card games na online slots.

Baadhi ya michezo ya slot games za kawaida katika kasino ya Betway ni kama Age of Discovery, High Society, Break Da Bank, Mega Money Multiplier na Riviera Riches. Mingine ni Football Star, Adventure Palace HD, na Thunderstruck.

Katika kasino ya Betway, kuna baadhi ya aina za slot games ambazo ni kama zile za kisasa na zile za kifahari. Vile vile, kuna nyingine ambazo huwa na nafasi ya kutazama filamu na maigizo ya kuchekesha.

Sehemu ya michezo hii ya kimtandao inakupa baadhi ya sifa za kifahari. Hivyo, una uhuru wa kuchagua iwapo utacheza michezo rahisi au ile changamano.

Tembelea Casino ya Betway


Bakshishi ya Michezo ya Kasino nchini Kenya-Inapatikana?

Bakshishi ya Michezo ya Kasino nchini Kenya haipatikani kwa sasa. Hata hivyo, kampuni hii iaangazia suala la kuwapa wana kasino bakshishi hii . Sisi tutazidi kukupasha zaidi kama kutakuwa na mabadiliko yoyote hivi karibuni.


Michezo ya Kuwekeza Dau almaarufu Betgames

Sehemu ya BetGames

Wakati mwingine unatamani sana kuwekeza dau hata baada ya firimbi ya kutamatisha kupulizwa. Ili kuweza kujipatia fursa kama hii, Betway Kenya inakupa michezo ya betgames ili uendeleze uchezaji wako unaokupa matokeo ya michezo kwa haraka. Hii michezo huhusisha kiolesura kizuri mtandaoni kinachowezesha kubihi fedha kwa michezo ya moja kwa moja.

Baadhi ya betgames unzoweza kucheza katika Betway Kenya ni kama Casino Classic, The Dice, pamoja na Wheel Fortune Games.

Ili kuweza kushiriki katika michezo hii ya Betgames nchini Kenya, unahitaji kuingia katika akaunti yako na baadaye uitembelee sehemu ya betgames na kuchagua mchezo uupendao kabla ya kuwekeza dau lako. Kisha mwishowe, bonyeza panapoonyesha ‘Wekeza dau’


Kuweka na Kubihi Fedha kwa Wateja wa Betway nchini Kenya

Wakenya wanaoshiriki kamari katika Kampuni ya Betway humu nchini wana baadhi ya njia za kuweka na kubihi fedha zao wanapocheza uwekezaji dau. Njia zilizo na umaarufu katika kuweka fedha kwenye akaunti za kucheza kamari ni kama huduma za pesa kwenye rununu. Baadhi ya njia hizi ni M-Pesa na Airtel Money. Licha ya hayo, unaweza pia kuzitumia kadi zako za benki.

Katika upande wa kubihi fedha zako, unaweza kukamilisha shughuli ya kufanya hivyo ukitumia njia uliyoitumia kuziweka kwenye akaunti yako peke yake.

Jedwali linalofuata hapa chini linaonyesha masharti pamoja na viwango vya njia tofauti za kuweka na kubihi pesa katika Betway Kenya;

Payment MethodDeposit MinimumDeposit MaximumTime for Deposit
Airtel LogoAirtelKSH 10KSH 70 000Immediate
M-Pesa LogoM-PesaKSH 10KSH 70 000Immediate
Visa LogoVisaKSH 10KSH 70 000Immediate
MasterCard LogoMasterCardKSH 10KSH 70 000Immediate
Payment MethodWithdrawal MinimumWithdrawal MaximumTime for Withdrawal
Airtel LogoAirtelKSH 80KSH 70 00/per dayup to 24 hours
M-Pesa LogoM-PesaKSH 80KSH 70 00/per dayup to 24 hours
Visa LogoVisaKSH 80KSH 70 00/per dayup to 24 hours
MasterCard LogoMasterCardKSH 80KSH 70 00/per dayup to 24 hours

Programu ya Rununu ya Betway

Toleo la simu ya Betway

Kwa wakati kama huu ambao mchezo wa kamari umechukua mkondo wa kimtandao, Kampuni ya Betway Kenya imebuni programu ya rununu kwa wateja. Programu yenyewe imeundwa kwa simu zitumiazo Android na pia iOS.

Ina kiolesura kizuri na cha kupendeza mno kwa wacheza kamari wa humu nchini Kenya. Mwanzo, iina rasimu nzuri na nyepesi mno kutumia. Bali na haya, ina mwangaza mzuri na inaleta matokeo kwa kasi mno. Zaidi na haya, programu hii ya rununu inakupa nafasi anuwai za kucheza kamari yako na kuwekeza dau. Kila wakati, unapokea jumbe za kukuarifu lolote ambalo linatukia katika akaunti yako na uwanjani vile vile. Miongoni mwa jumbe hizi ni zile zinazohusu mechi na michuano, bakshishi za Betway pamoja na ofa mbali mbali.

Unaweza kuidungua programu hii ya Betway katika platifomu mbali mbali kwenye mtandao.


Programu ya Ushirika

Betway Kenya ina programu ya ushirika ikishirikiana na Betwaypartnersafrica. Programu hii inamilikiwa na kuendelezwa na mataifa sita ya Kiafrika ambayo ni Uganda, Afrika ya Kusini, Ghana, Kenya, Zambia na Nigeria.

Katika mpango huu wa ushiriki, unapewa vifaa vya kufanyia Betwaypartnersafrika matangazo ya kibiashara ili kupata wateja watakaojiunga na Betway kupitia kwako. Pindi tu wanapojiunga na kujisajili kwa kiunga au ushirikishi wako, unapata kamisheni.

Katika mpango huu, utaweza kujipatia asilimia 25 ya kipato cha Betway kutokana na mteja wako mpya uliomleta.

Ili kujiunga na programu hii ya kuhusisha, lazima ufuate sheria na masharti yafuatayo;

 • Lazima uwe umetimiza umri wa miaka 18 kwenda juu
 • Lazima upeane habari kamilifu na ya kweli inayokuhusu wewe binafsi
 • Hutajaribu kubadilisha au kurekebisha vifaa vya kufanya matangazo ya kibiashara vya kampuni ya Betway
 • Kwamba wateja uliowaelekeza kwako lazima wawe na chapisho lako la kuonyesha ni wewe uliowaelekeza kujiunga na Betway
 • Kwamba shughuli zote za wateja wako lazima zikaguliwe kabla ya kipato chako cha kuwaelekeza wateja kikadiliwe
 • Kwamba utatumia vifaa vya kufanya matangazo ya kampuni kwa njia inayoonyesha utiifu wa sheria
 • Kwamba hutatuma jumbe, baruapepe au aina nyingine yoyote ya mawasiliano kuhusiana na Betwaypartnersafrica bila kibali
 • Kwamba shughuli zako zote zitaonyesha ufuasi na utiifu wa sheria zote zionazotawala ulingo wa michezo ya Kamari

Waama, masharti haya ni mapana.ili kuhakikisha uhusiano mzuri kati yako na wateja ambao utawaelekeza kwa Betwaypartnersafrica. Hivyo, ni bora Zaidi kuangazia sheria na masharti haya kwa kina kabla ya kujiunga na mpango huu ili kuhakikisha utayafuata.


Maswali Yanayoulizwa kwa Wingi

Baadhi ya maswali yaliyoulizwa kwa wingi kuhusiana na Betway Kenya ni kama yafuatayo;

Nitaweka pesa vipi?

Unafaa kuingia kwenye akaunti yako na hapa utaweza kupata nafasi ya ‘weka’ pesa. Baadaye, chagua njia ya kuweka pesa na kisha ufuate hatua ulizotolewa.

Baada ya kushinda, itachukua muda gani ili pesa zangu ziwekwe kwenye akaunti?

Fedha zako za ushindi wa kuwekeza dau zinawekwa kwenye akaunti yako moja kwa moja. Hata hivyo zinaweza zikachelewa kwa muda wa hadi saa 48 kama kuna hitilafu ya mtandao. Hatimaye, pesa zinaweza kurejeshwa kwa mhudumu wako wa pesa za rununu.

Pesa ninazobihi zitawekwa wapi?

Pesa unazobihi baada ya ushindi hutumwa kupitia ile nambari uliyoitumia wakati wa kuwekeza dau. Ukweli ni kwamba huwezi hata kubadilisha nambari ya rununu iwe tofauti na ile uliyosajilishwa nayo.

Utoaji wa mapema almaarufu early settlement ni nini?

Huku ni kule kutoa pesa zako kabla michuano yote kukamilika katika mchezo wa jakpoti.

Nitashinda kiwango gani cha pesa nikiweza kutabiri michuano yote kwa njia sahihi katika jakpoti?

Ukiweza kufanya utabiri wa kweli wa michuano yote katika jakpoti, utapokea kiwango chote cha fedha katika jakpoti hiyo. Kama ilikuwa jakpoti ya watu wengi, pesa hizo zitagawanywa miongoni mwa washindi wote.

Je, Betway ni kampuni iliyosajilishwa nchini Kenya kweli?

Naam, Betway ni kampuni iliyosajilishwa nchini Kenya. Ilisajilishwa na BCLB mwaka wa 2015 chini ya leseni nambari 829.

Ni umri upi uliokubalika nchini Kenya ili nikubalishwe kushiriki kamari na uwekezaji dau?

Umri uliokubalika kisheria nchini Kenya ni miaka 18.


Usaidizi wa Wateja

Betway Kenya ni kampuni ambayo ina timu nzuri ya watu wanaowasaidia wateja kujibu maswali na matakwa yao.Unaweza kuwafikia kwa mazungumzo yoyote yale kuanzia jinsi ya kuweka fedha, kuwekeza dau, kubihi fedha baada ya ushindi na mengineyo. Angalau hatukupokea lalamishi lolote kuhusu wasaidizi wa wateja katika matayarisho ya muhtasari huu.


Njia za Kuzungumza na Betway Kenya

Unaweza kuifikia Betway Kenya kwa njia yoyote miongoni mwa hizi;

Vile vile, unaweza kuzungumza nao kupitia Live Chat.


Hitimisho na Makadirio ya Ubora

Betway ni mojawapo ya kampuni za kamari nchini. Imejipatia umaarufu anuwai katika soko hili la kamari hapa Kenya na katika baadhi ya mataifa ya Afrika.

Kwa sababu ya uwezo wa kumiliki simu za rununu miongoni mwa watu wengi nchini Kenya, umaarufu wa Betway pamoja na kampuni nyingine za kamari unaendelea kuenea. Vile vile, kuna mabadiliko makubwa yanayotarajiwa kwa muda wa siku chache. Jambo hili linatokana na uwepo mkubwa wa kampuni za kamari na vitumizi vyao.

Betway Kenya kama mojawapo ya kampuni za kamari huku nchini Kenya, ina makadirio ya ubora ya 9/10.

Jiunge na Betway

Betting expert Elica Martinova
Certified Betting Expert
Elica Martinova
Ellie is in charge of writing, editing, and publishing reviews in Bulgarian, English, and German. She has a long track record as a journalist and is passionate about writing. Also, she is quite experienced when it comes to bookmakers as well.